JINSI YA KUTUNZA MIKO YA KUPIKIA

Mwiko ni kitu kidogo sana jikoni lakini ni kifaa muhimu sana katika mapishi. Katika mapishi yote unayopika Mwiko lazima utumike , ila mara nyingi wengi huwa hatuoni umuhimu wa miko sababu tu ya udogo wake. Ila tuko busy kutunza vyombo vingine ila miko tunasahau. Hivyo pia ni lazima kuzingatia usafi na utunzaji wake;

1.Osha mwiko wako pale pale unapomaliza kupika, usiuache ukae masaa mengi haujasafiswa, ukimaliza ukaushe na kitambaa kisha uweke upate hewa. Ukiacha miko muda mrefu bila kuosha inaweka harufu .

2.Usipende kuloweka mwiko, maana umetengenezwa kwa mbao unaoloweka mara kwa mara utaufanya uchakae haraka au hata uanze kuoza.

3.Paka mafuta miko yako (olive, alizeti nk) kuzuia isipauke haraka na kufubaa, walau kwa mwezi mara moja. Unaupaka mafuta kisha unauacha kwa usiku mzima, asubuhi unaosha na kufuta na kitambaa.

4.Ukiona mwiko unatoa harufu zisizo eleweka ukamulie ndimu kisha futa na kitambaa inasaidia kupunguza harufu.

5.Ni vizuri kuweka miko yako sehemu moja tafuta jug kubwa au chupa kubwa yenye mdomo mpana, uwe unaweka miko yako ndani kwa pamoja sio Ukitaka kupika sio kutafuta mwiko uko wapi.

6.Mwiko ukishapasuka utupe haufai tena usiendelee kutumia.

Mwiko ukitunzwa vizuri unadumu sana na unakuwa unapendeza, hata ukiutumia jikoni unaufurahia. Wewe je unautunza vipi mwiko wako?