DOUGHNUT RECIPE

Jana jioni nilijaribu kutengeneza doughnut kwa ajili ya chi ya jioni, ndio ilikuwa mara ya kwanza maana huwa siku zote nanunua, zilitoka vizuri na zilikuwa tamu. Recipe hiyo hapo chini;

Mahitaji

Ngano 300 gm
Sukari vijiko vikubwa vinne
Margarine/blueband vijiko viwili vikubwa
Maziwa 200 ml
Chumvi kijiko kidogo nusu
Hamira kijiko kidogo kimoja
Mayai 2
Mafuta kama robo lita ya kukaangia

Jinsi ya kutengeneza

  1. Weka hamira kwenye bakuli kisha tia maji vijiko vikubwa 3 na ikoroge mpaka ichanganyike vizuri
  2. Pasha maziwa moto yawe ya uvuguvugu
  3. Chukua bakuli ya kukandia weka sukari kisha tia yai na changanya vizuri vichanganyike kwa kutumia mwiko au whisk ,
  4. Kisha tia margarine na endelea kuchanganya vizuri
  5. Kisha tia unga, na hamira na maziwa na kanda mpaka ngano imeshikana yote kama donge
  6. Acha kama dakika 15
  7. Baada ya hapo sukuma donge lako la ngano kutengeneza duara kama chapati
  8. Kisha anza kukata ngano kwa kutumia cookies cutter yenye umbo la duara ili kupata viduara vidogo vidogo, kisha tumia chupa yenye mdomo mdogo kutengeneza kiduara kidogo chenye shimo katikati yake.
  9. Kisha acha ngano iumuke kama masaa mawili kisha unaweza kukaanga acha ibadilike rangi kuwa brown kisha geuza upande wa pili iive kisha unaweza kutoa, zitakuwa tayari.
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s