SIMPLE BISCUITS


 

Leo nitakwenda kuelezea jinsi ya kutengeneza simple biscuits, ni rahisi sana kutengeneza na inatumia muda mfupi sana.

Mahitaji;
-Ngano- robo kilo (250 gram)
-Sukari- vijiko 5 vya kulia chakula
-Siagi- vijiko 3 vya kulia chakula
-Mayai 2 makubwa

-baking powder kijiko 1 cha chai

Vifaa utakavyotumia;
-Rolling pin(ya kusukumia chapati)
-Mwiko
-Kibao cha kusukumia chapati / au kukatia vitu jikoni
– Biscuits cutter/ au unaweza kukatia na kisu
-Bakuli kubwa (Mixing bowl)

Jinsi ya kutengeneza

1-Weka sukari kwenye bakuli

2- Halafu weka Siagi, kisha changanya Siagi na sukari kwa kutumia mwiko mpaka vichanganyike
Weka mayai na endelea kuchanganya na mwiko, Kisha weka ngano na baking powder changanya vizuri kisha uanze kukanda

3 – Ukimaliza kukanda unga , gawanya Vitoke viduara vitatu, chukua kiduara kimoja kimoja weka katika kibao chako sukuma ( kama chapati) kisha chukua biscuits cutter kama unayo au hata kisu, anza kukata maumbo unayotaka.

4 – weka biscuits kwenye baking tray, ziweke pembeni, wakati ukisubiri oven ipate moto.

5 – Washa oven yako, moto 150C/390F subiri zipite dakika tano, kisha weka biscuits.

Ziache ndani ya oven dakika kama 15, au kama unataka zikauke zaidi ziache dakika ishirini.
Baada ya hapo biscuits zitakuwa tayari, zitoe nje ya oven na ziache kidogo zipoe, baada ya hapo zitakuwa tayari kuliwa.

Mengineyo;

Simple biscuits hizi unaweza kunywea chai, kahawa ,maziwa au hata juisi na vinywaji vingine utakavyopenda.

Advertisements