MISHIKAKI – jinsi ya kuweka viungo

Mishikaki unaweza kutengeneza kwa kutumia nyama tofauti tofauti, mishikaki ya kuku, samaki, ng’ombe, mbuzi kitimoto nk. Lakini kutengeneza mishikaki mitamu yenye ladha nzuri siri iko kwenye viungo utakavyo tia kwenye nyama .

image

Ili kupata mishikaki yenye ladha nzuri ukishaweka viungo kwenye nyama unatakiwa uiacha kwa masaa kama nane ndio viungo vinakoleà vizuri, sio kuweka hapo hapo kisha unachoma.

Osha nyama ya kutengeneza mishikaki, kisha katakata vipande vya wastani( visiwe vikubwa sana au vidogo sana), weka kwenye bakuli kisha tia chumvi, limao.

image.jpeg

‘Chukua tangawizi, kitunguu saumu, binzari nyembamba, pilipili manga na pilipili mbuzi. Twanga pamoja kisha changanya katika nyama , changanya vizuri. Weka nyama katika fridge, kwa masaa nane au usiku mzima. Pilipili kama una watoto unaweza kutengeneza pembeni badala ya kuweka moja kwa moja.

image

Kisha ndio unaweza ukuchoma kwenye mkaa au oven, kwa hiyo kama unataka kula mishikaki mchana andaa nyama usiku. Kama unataka kula jioni andaa nyama asubuhi jioni unachoma. Unaweza kuweka viungo vyovyote unavyotaka.

Unaweza kula mishikaki na ndizi chôma, chipsi, pilau, ugali nk pia ukatengeneza kachumbari au salad Ukitaka ufurahie zaidi.

Advertisements