USHAURI( ask for advice)

Kwa ushauri wowote ule niandikie, email: eunicemahundi@yahoo.com, WhatsApp: +33753832124, au unaweza kuandika katika comment. Jina lako  halisi wala taarifa zako binafsi kama simu, email havitawekwa hapa, usiri utazingatiwaimage

7/11/2015

Dada habari za kazi? Mimi ni meolewa siku za karibuni, lakini kuna kitu kimoja hakinipi amani. Mume wangu mimi anataka  nimfulie mpaka nguo zake za ndani, nikwambia afue mwenyewe anasema hawezi kusitakatisha. Nimemuuliza kwani zamani alikuwa anakufulia nani? Anasema ya zamani yamepita, we mke wangu upo utanifulia. Sasa mimi kweli naona shida kufua chupi za mtu mwingine sijui nifanyeje?

xoxo

Ndugu yangu xoxo; Kama amesema anashindwa kuzifua vizuri, si mbaya kama ukamsaidia Maana ni mumeo na mmeshakuwa mwili mmoja. Usilifanye kuwa tatizo kubwa kiasi hicho cha kukosa amani, ndoa yenyewe bado changa yaani kutofautiana kisa kufua vyupi? Au Kama unaona ni tatizo kubwa kwako kiasi hicho, basi kaa chini na mumeo muongee muone mtafanyaje.

Eunice

———////////—————————–//////———————————————–//////////—//////////////////////-/——–

20/10/2015

Dear dada eunice; nisaidie natamani nichukue mkopo wa biashara lakini naogopa naona mkopo muda wa kuanza marejesho ya mkopo  baada ya kuchukua ni mfupi sana, pia sijui hata nifanye biashara gani. Nilikuwa nafikiria kufunga kuku au biashara ya vinywaji, bado sielewi.

-jina limehifadhiwa

Kwanza kabisa ni vizuri kuanza biashara kama unaweza hata kwa mtoaji mdogo lakini si mkopo, kuanza biashara yako kidogo kidogo kadiri unavyopata faida unapaua biashara yako.

Mkopo ni mzuri ikiwa una uhakika biashara unayofanya itaenda vizuri ,utapata faida na kurudisha hela ulizochukua. Pia Pili kabla ya kuchukua mkopo unatakiwa uwe na akiba  nyingine pembeni au mtu unayemtegemea, kama biashara haitaenda vizuri una uhakika wa kufanya marejesho ya mkopo is tena kuanza kuangaika.

Tatu kabla ya kuchukua mkopo unatakiwa uwe tayari unajua biashara gani unaenda kufanya, wapi itafanyika na wateja wako utawapata vipi, lazima uwe umejipanga. Kwa wewe naona unahitaji muda kidogo kufanya utafiti wa biashara unayotaka kufanya kabla ya kuamua kuchukua mkopo.

Nne hizo biashara ya kufuga kuku na vinywaji baridi, lazima ukumbuke pia zinategema umeme kwa kiasi fulani, kuku usiku wanahitaji taa, na umeme ukiwa wa mgao lazima ufikirie utafanyaje?

bora kama unao mtoaji wa kwako kidogo uanze biashara mwenyewe bila mkopo, itakuwa vizuri zaidi ukishajipanga ndio uangalia uwezeakano wa mkopo.

Eunice

———————————-/////—————————————————–//////////————————————

8/10/2016

Habari dada Eunice, mi kuna kitu kinanikera unakuta mtu anakuja kwako kukutembelea, unamkaribisha kwa mikono miwili na moyo mweupe, sasa akiondoka anaenda kukusema vibaya kwa watu ooh nimeenda kwake nimemkuta kachoka mbaya hata soda kashindwa kuninunulia, nimeishia kula ugali na maharage, mara ooh yani nimemkuta makochi yale yale tuliyomtunza kwenye kitchen party 2010 mpaka leo hajabadilisha,na maneno mengine mengi  unayasikia kwa watu, hivi dada mtu kama huyo unamfanyaje?

-jina limehifadhiwa

Ndugu yangu kwanza pole sana kwa yaliyo kukuta, ushauri wangu mtu kama huyo ni kumwambia ukweli. Mwite kwako au mpigie simu  uongee naye, mwambie tabia yake haijakupendeza hata kidogo na sio ustaarabu alichofanya. Mambo ya nyumbani kwako na maisha yako ni mambo binafsi hana haki ya kuyasambaza kwa watu, mwambie kama anataka mahusiano yaendelea kati yenu aache tabia ya umbea, maana hata yeye akifanyiwa hivyo hatafurahia. Kama ataomba msamaha, vizuri maisha yanaendelea, ukiona haelekei kuelewa anataka ugomvi achana naye, kila mtu akae kwake.

Eunice

~~~~~~~~~~,~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

24/09/2015

Ana (sio jina halisi);  anauliza  Jifanye nini ili wazazi wangu wasiniingilie katika maamuzi au mambo mbalimbali katika maisha yangu? Mimi ni madada mkubwa tu sijaolewa bado ila najitegemea kwa kila kitu, na naishi maisha ya kujiheshimu sana. Tatizo ni wazazi wangu wanataka waniingilie kwa kila nalofanya, wananichagulia marafiki, wananipangia hela zangu nitumie vipi nk, kwa kweli wanikera sana.

Ana nimekuelewa, kitu cha kwanza unachotakiwa kufanya ni kukaa chini na kuongea na wazazi wako kama mtu mzima. Waaambie kwamba wewe sasa ni mtu mzima mwenye akili timamu na una haki ya kufanya lolote unalotaka, wazazi wako kwa sasa wana yakiwa kuwa ni washauri kwako kwa lolote lile wanaloona  litaweza kukusaidia, na utaamua mwenyewe kuchukua au kutochukua ushauri wao. Waeleze ukweli kuwa unakwazika, na kama wangependa mahusiano mazuri na wewe basi wasiingilie na kukulazimisha nini cha kufanya katika maisha yako maana wewe si mtoto chini ya miaka 18, naamini watakuelewa. Kila la heri.

Eunice

Advertisements

2 thoughts on “USHAURI( ask for advice)

  1. Habari dada mimi jiko langu kubwa mno nashindwa naomna ya kulipanga hata kuvutia naomba nishauri jinsi ya kupanga liwe na mvuto.

    Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s